MOHAMED IBRAHIM MO BADO ANAAMINI KATIKA MUDA NDANI YA KIKOSI CHA SIMBA.
UKIACHANA na lile jina la Mohamed
Ibrahim 'MO' yule Mfanyabiashara mashuhuri, Simba wana mchezaji wao dhahabu anayejulikana kwa
jina la Mohamed Ibrahim 'MO'. Hawa ni MO wawili tofauti kabisa.
MO mmoja ameamua kuwa mfanyabiashara
na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa, ilihali MO mwingine ameamua kuwa mcheza mpira, lakini
mambo yake hayaonekani kwenda sawa.
Leo tutamzungumzia zaidi MO
mchezaji, MO na ukimya wake kama alivyo anapambana na utitiri wa viungo
ili kulishawishi benchi la ufundi la wekundu wa msimbazi simba limuamini licha ya kuwa Hajaonekana kwa muda sasa akicheza.
Kutokuonekana kwake haina maana ana
majeraha, au anamatatizo ya kifamilia, La hasha! Ni mzima wa afya na hana matatizo ya
kifamilia wala majeruhi, ila utitiri wa viungo umemfanya pole pole aanze kupotea kwenye mboni za
macho ya wadau wa soka letu. Inasikitisha sana.
Mashabiki hawana muda naye tena na hakuna
anayehoji wapi aliko kwa sasa kwa Sababu kuu moja tu ambayo ni simba kuwa inafanya vyema hivi sasa ilivyo kwa MO ni sawa na mashabiki wa simba kutohoji kukosekana kwa kiuongo mnyumbulifu awapo uwanjani Haruna Niyonzima kwa muda mrefu, vipi wahoji
kukosekana kwa MO?
Hapana shaka kusema Simba wana kikosi kipana msimu huu, Pengine timu ingekuwa inafanya vibaya jina la MO lingalikuwa likitamkwa na angalitoka
huko kusikojulikana na kila wiki tungalimuona sehemu ya kikosi cha wekundu wa msimbazi simba kama sehemu ya wachezaji 11 uwanjani au
wachezaji wa akiba.
Lakini Simba hii yenye kikosi ghari zaidi kwenye ligi kuu soka Tanzania bara yenye kuchagizwa na nguvu kubwa ya uwekezaji wa mfanyabiashara kijana na mashuhuri barani afrika, siyo Simba
ya msimu uliyopita iliyokuwa ikiungaunga kupata matokeo chanya, Simba hii kama haupo na lako halipo zaidi ni kuendelea kusubiri malipo ya jasho litokalo wakati wa mazoezi yanayojumuisha kikosi kizima huku baadhi yao wakilipwa kwa jasho la dakika 90 za mapambano ya uwanjani Ni rahisi kusema hivyo na ni dhahiri kuwa MO anakutana na ugumu
huu ndani ya kikosi cha simba.
Mara kadhaa nimewahi kuwasiliana naye
pengine kufahamu ni nini kinamfanya asitumike katika kikosi cha kwanza majibu yake hayana tofauti na majibu ya mchezaji aliyecheza michezo yote ya ligi kuu vpl msimu uliopita niliyemsikia usiku mmoja katika kituo kimoja cha radio akizungumzia mustakabari wake ndani ya kikosi hicho ikimbukwe ndiye aliyetangazwa kuwa mchezaji bora wa VPL 2016/17 naye si mwingine ni Mohamed Hussein maarufu 'Tshabalala', Majibu ya Mo kuhusu kukosa nafasi hayana tofauti na 'Tshabalala, Mo anasema Ukosefu wa nafasi ndani ya kikosi cha simba ndiyo unamfanya asionekane uwanjani mara nyingi msimu huu.
Kadhalka Ananiambia kukosa nafasi ndiko
kunakomfanya asionekane uwanjani, lakini hana majeraha yeyote yale pengine kama yanayowakumba baadhi ya wachezaji pale upande wa pili wa shilingi kwa mahasimu wao pale jangwani.
Kauli hii inapaswa kufikiriwa kwa upana wake zaidi, Ni kweli nafasi inamfanya tushindwe kumuona MO mwenye sifa ya
kuufanya mchezo wa mpira wa miguu kuwa rahisi mbele ya macho ya wadau wa soka nchini na mpira kumtii.
Licha ya wakati mgumu anaokutana nao
Mo ndani ya wekundu wa msimbazi Simba, binafsi naamini katika muda.
Muda wake bado haujafika, kwani
muda ukifika hakuna wa kumzuia. Hapo nadhani wengi tutaanza kubadili mikao yetu
kwa ajili ya kumtazama namna anavyourahisisha mpira na kuonekana kuwa mchezo rahisi sana katika macho ya watu.
Hapo hatutamtazama kwa macho haya
tunayomtazama sasa, tutamtazama kwa jicho la tatu na pengine tutajiuliza kwanini
alichelewa kupewa nafasi ya kucheza mara nyingi zaidi katika kikosi cha simba Tuendelee kuamini
katika muda ili kumuona MO kwa mara nyingine tena.
Muda huu ambao Simba imeenea na
kuzitawala mechi nyingi wanazocheza, kwa kupata matokeo chanya kwenye ligi kuu soka Tanzania bara tunahitaji muda ili tumuone MO yule anayetajwa na baadhi ya wachambuzi wa soka kuwa na tabia ya kuufanya mchezo wa mpira wa miguu kuonekana kuwa rahisi kwa wadau.
Post a Comment