SABABUA YA CHIRWA NA KAMUSOKO KUACHWA KWENYE MCHEZO DHIDI YA St. LOUIS YA SHELISHELI.
KIKOSI cha Yanga Sc kinatarajia kusafiri Leo asubuhi kueleka
Shelisheli tayari kwa mchezo wa marejeano na wenyeji St Louis Fc kwenye
ligi ya mabingwa afrika mchezo uliopangwa kuchezwa Jumatano ijayo Stade
Liete.
Siku ya Jana Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa
jumla ya nyota 20 na viongozi 10 kati yao nane kutoka benchi la ufundi
watasafiri asubuhi ya kesho kupitia Nairobi tayari kwa mchezo huo
muhimu siku ya Jumatano.
Maandalizi yote muhimu yamekwisha fanyika, timu imefanya mazoezi ya mwisho leo tayari kwa safari hiyo. Kwenye kikosi nyota waliyokuwa na majeraha ya muda mrefu kama Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Abdallah Shaibu na Yohana Mkomola wataendelea kukosekana hii ni kwa sababu bado wanauguza majeraha,kucheza ugenini kunachangamoto zake lakini tumejiandaa vizuri kwa sababu tushacheza nje mara nyingi hivyo hakuna hofu kati yetu.
Akiendelea zaidi Ten amesema kuwa, mchezaji Thabani Kamusoko ambaye
amepona majeraha yake hivi karibuni na kuanza mazoezi mepesi,ameondolewa
kutoka orodha ya nyota ambao wangesafiri kueleka Shelisheli ili apate
muda wa kujifua zaidi na kurejesha makali yake, mchezaji Obrey Chirwa
pia hayumo kwenye orodha hiyo kwa sababu ya maumivu ya misuli.
Ilikuwa asafiri kuelekea Shelisheli, lakini imekazimu benchi la ufundi kumuondoa kwa sababu bado hajawa sawa asilimia 100, anahitaji muda wa kujifua zaidi ili kupata utimamu wa mwili tayari kwa mapambano uwanjani , daktari wake pia amethibitisha kuwa mchezaji anatakiwa apate muda wa kujiweka sawa kabla hajaanza kucheza mechi kulingana na majeraha aliyokuwa nayo.
Orodha kamili ya wachezaji ambao safiri kuelekea Shelishelini kama Ifuatavyo:
Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya, Youthe Rostand, Hassan Kessy, Juma
Abdul, Mwinyi Haji, Gadiel Michael, Nadir Hariub, Patto Ngonyani,
Kelvin Yondani, Said Juma, Papy Tshishimbi,Pius Buswita, Raphael Daud,
Yussuf Mhilu, Ibrahim Ajib, Said Mussa, Emmanuel Martin, Godffrey
Mwashiuya, Juma Mahadhi.
Post a Comment