AMMY NINJE ASEMA MNIACHE NIFANYE KAZI YANGU MTAONA MATOKEO
Kocha wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya Miaka 20 "Ngorongoro Heroes" Ammy Ninje amesema, katika kuhakikisha kikosi chake kinafanya vizuri katika mchezo wa marudiano dhidi ya Dr Congo na kuhakikisha wanasonga mbele katika michuano ya kuwania kufuzu AFCON U20 amefanya ongezeko la wachezaji wawili huku akiwataka mashabiki kuacha kulaumu juu ya upangwaji wa kikosi cha kwanza bila kujua lengo la kocha.
Kocha Ninje amesema, licha ya kufanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa awali lakini aliona ni namna gani anaweza kuongeza wachezaji ambao anaamini wataleta mabadiliko kwenye kikosi kwa kuwaongeza Habib Kyombo kutoka Mbao pamoja na Rashid Chambo aliyekuwa akifanya majaribio Nchini Sweden ambao anaamini kwa kushirikiana watafanya vizuri katika michezo iliyombele yao ambapo wanatarajia kuondoka Aprili 18 au 19.
"Tuliona mapungufu katika mchezo ya Kwanza dhidi ya Dr Congo ambayo tulishambulia sana lakini hatukupata nafasi ya kufunga magoli kwahiyo tunafanya mazoezi kujaribu kusaidia washambuliaji na wachezaji wa katikati kupata muunganiko mzuri, kwahiyo maandalizi yanaendelea vizuri kwaajili ya mchezo wa marudiano, " amesema.
Kocha Ninje amewataka pia watanzania kubakia kuwa watazamaji tu na sio kutoa lawama pale timu inaposhindwa kufanya yale wanayoyataka kwa muda ule bali waache wahusika kwani wanajua ni nini wanatakiwa kufanya na mchezaji gani anatakiwa kupangwa kwa wakati gani.
"Mashabiki watabakia kuwa watazamaji na mimi ni Mtaalamu sasa siwezi kuwasikiliza watu ambao hawajasomea Soka, mimi ndiye ninayekaa na wachezaji na najua nani anafanya viziuri wachezaji nani anafanya vizuri mazoezini na nani hafanyi vizuri mazozini, sasa ukiwasikiliza wasiojua mpira utakuwa unakosea, " amesema.
Kwa upande wake Mshambuliaji Habib Kyombo amesema, anaamini mchanganyiko wa wachezaji unaofanywa na benchi la ufundi la Ngorongoro Heroes utaleta matokeo mazuri ambayo yataweza kuwafikisha pale wanapopatarajia.
"Nimejiunga kwenye kikosi kuongeza nguvu naamini tutafanya vizuri kutokana na muunganiko ambao umefanywa, naamini kutakuwa na ushindani lakini tunajitahidi kupokea mazoezi ya Mwalimu ili tuweze kufanya kile kinachotakiwa ili kuweza kusonga mbele, " amesema.

Post a Comment