KESI YA MALINZI NA WENZAKE,YASOGEZWA MBELE TENA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele tarehe ya  kuwasomea maelezo ya awali (PH) vigogo watatu wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hadi Aprili 18/2018.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa serikali, Shedrack Kimaro kuitaarifu mahakama kuwa wanaomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka kwanza ndiyo waendelee na PH.

Wakili Kimaro amedai, "kesi leo imepangwa kwa ajili ya PH, Mimi ndiyo nimepangiwa kuendelea na kesi hii, nimefanya Mawasiliano na (Takukuru) tukapitia ushahidi uliokusanywa hivyo tunaomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka Kwa kuongeza washtakiwa wengine ndiyo tuendelee na PH" ameeleza..

Maelezo hayo ya awali leo yalipaswa kusomwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Kimaro aliendelea kudai kuwa mmoja wa washtakiwa wanaopaswa kuunganishwa kwenye kesi hivyo yupo nje ya Dar es Salaam na utaratibu wa kumleta umekamilika.

Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Mashauri aliiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 18,2018.

Watuhumiwa katika kesi hiyo ni, aliyekuwa Rais TFF, Jamal  Malinzi(57), Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine(46) na Mhasibu, Nsiande Mwanga(27)

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418. 7

Katika kesi hiyo, Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 28 ya uhujumu uchumi ikiwamo kughushi na utakatishaji wa fedha dola za marekani 375,418.

No comments