Makala:Klalamu huru ya mjukuu wa Mkeyenge


Na:Abdu Mkeyenge

WIKI moja iliyopita tuliwaona fans wa Juventus wakiinuka vitini mwao kumpigia makofi Ronaldo aliyewaadhibu kwa bao la bicycle kick. Hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kuinuka vitini na kufanya walivyofanya.

Wakati mwingine unapata mzuka wa kupiga makofi, bila kujali nani unayempigia hayo makofi yenyewe. Fans wale hawakuwa wajinga. Ronaldo alistahili kupigiwa makofi. Wenzetu sio wanafiki.

Waliishuhudia timu yao ikilala 3-0 tena katika ardhi yao ya Turin. Hatukuona hata chembe ya lawama kwa wachezaji, kocha wala mwamuzi. Wenzetu ndio wako hivi. Wakishinda wanashinda pamoja, wakishindwa wanashindwa pamoja.

Wakarudi tena uwanja wao wa mazoezi, wakajifua kadri walivyojifua, leo wamerudi tena uwanja wa mechi kucheza dhidi ya Ronaldo na wenzie. Game mpaka dakika 90+2, Juventus wako mbele kwa mabao 3-0. Hii ni copy na kupaste ya kile kilichofanyika Turin katika wiki ya jana.

Katika mshangao wa ajabu kabisa mwishoni mwa mchezo mwamuzi Michael Oliver anaifanya game ikose radha na yeye ndiye anaenda kuibuka man of the match. Anatoa tuta 'tata' na anamtoa nje kwa kadi nyekundu Buffon. Ronaldo anachukua mpira na kutia kimiani, Madrid inasonga mbele.

Ghafla Santiago Bernabeu inageuka uwanja wa ngumi, kumbe ni uwanja wa mpira. Wachezaji Juventus, staff wao wanamfuata Oliver na kumzonga. Hapa tunapaswa kujiuliza kwanini hawa Juventus wamgande mwamuzi leo hii walalamike, wakati game iliyopita fans wake walinyanyuka vitini kutoa heshima kwa Ronaldo? Kuna kitu!

Why Buffon apate 'umeme' kwa kuhoji? Kama hajaenda kuhoji Buffon ambaye ndiyo nahodha wa timu, nani mwingine aende? Nadhani kwa pamoja tumepata majibu sahihi kwanini hakuna refa wa Kiingereza atakayecheza Kombe la Dunia Russia. Tumejionea wenyewe. Hatujahadithiwa.

Kuna ujumbe wameamua kuufikisha Juventus kupitia reaction zao, japo reaction zile haziendi kubadili kitu. Madrid imesonga, Juventus imebaki huu ndio ukweli uliosimama mpaka sasa.

Natamani Manara wa Juventus nae afanye alichokifanya Manara wa Simba. Manara wa Simba aliibeba tv yake nzima nzima na kuileta kwenye press. Wakati mwingine haya mambo yanachefua kuyaona hadi kuyasikia.

Anyway pichani ni kitoweo kinachoitwa Kambale. Hiyo ni nyama yetu kuu sisi Wandengereko. Ni kama wachaga wanavyokula visusio na sisi kususio chetu ndio hicho. Kalamu huru limeisha wino.

No comments