MAKOCHA TIMU ZA MIKOANI MCHEZO WA KRIKETI WAWEKA IMANI KWA WACHEZAJI WAO WALIOCHAGULIWA TIMU ZA TAIFA KUFANYA VIZURI MICHUANO YA KUWANIA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA

Mikoa shiriki katika Michuano ya Mchezo wa Kriketi kwa mikoa wanachama imesema kuwa wanaamini watapata timu bora za Taifa zitakazofanya vizuri katika mashindano ya kuwania kushiriki Kombe la Dunia kutokana viongozi wa Timu kuzoberesha zaidi timu zao tofauti na miaka iliyopita.


Kocha wa Kriketi kutoka Tanga Riziki Kisheto kwa upande wa wanawake wameshamaliza na wanaamini wachezaji waliochaguliwa ambao ni ongezeko kwa timu ya Taifa watafanya vizuri huku akiongeza kuwa mikoa mingi iliyokuwa haina uwezo wa kufanya vizuri kwa mwaka huu imeonyesha mabadiliko makubwa hali inayowapa imani kwa timu hizo kuweza kufuzu kuelekea Kombe la Dunia.


“Ukiangalia kiwango cha watoto kidogo kimeridhisha kwasababu mikoa ambayo ilianza zamani mchezo wa kriketi sasa hivi imepiga hatua kama ukiangalia kwenye Mkoa wangu wa Tanga ulikuwa nafasi ya pili kutoka mwisho lakini sasa hivi imekuwa nafasi ya Tatu kwahiyo naona kidogo maendeleo yapo kwahiyo naona kwenye timu ya Taifa watakaochaguliwa kwaajili ya kwenda Zimbabwe kutafuta tiketi ya kwenda Kombe la Dunia itakuwa nzuri zaidi, ” amesema.


Riziki amesema, hamasa ya viongozi wa Kriketi Taifa imechangia kwamikoa kufanya vizuri kwani walishauri Mikoa yote wanachama kuwa na mashindano ya Mikoa ya wasichana yatasaidia kukuza vipaji vya watoto na hatimaye kupata timu bora ya Taifa ya hapo baadaye.


Kwaupande wake Alide Morris ambaye ni Nahodha wa Timu ya wanaume kutoka Mkoani Mwanza amesema, kikosi kipo kamili kwaajili ya mashindano hayo ambayo kwa upande wa wanaume yameanza hii leo huku akiongeza kuwa muendelezo wa mazoeziwaliyokuwa wakiyafanya yameweza kuwajenga zaidi.


“Kwaupande wetu sisi tumejipanga vizuri na tunawaahidi tutafanya vizuri ili kuweza kutengeneza Timu nzuri ya vijana ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 19, na naamini kikosi kipo imara zaidi kwani mazoezi ambayo tumekuwa tukiendelea nayo yameweza kutujenga kwa kiasi kikubwa, ” amesema.


Alide ameongeza kwa kuwataka Watanzania na wadau wa mchezo huo kuendelea kuwapa sapoti kwani wanaamini watafanya vizuri katika mashindano makubwa yaliyombele yao.

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mchezo wa Kriketi

No comments