MTANZANIA ANAYEKIPIGA UJERUMANI EMILY MUGETA AREJEA RASMI DIMBANI BAADA YA MWAKA MMOJA WA KUUGUZA MAJERAHA
Baada ya kukaa nje ya dimba kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kuumia bega na kufanyiwa Upasuaji mara mbili hatimaye leo Emily Mugeta amerejea rasmi dimbani kwa kufanya mazoezi na timu yake asubuhi ya leo.
Akizungumza na Tiktaktz Mugeta amesema 'nashukuru mwenyezi Mungu kwa kuweza kurudi uwanja na pia ni jambo kubwa la furaha kwangu mimi na kwa timu pia baada ya kuanza mazoezi rasmi'.
Mugeta anayekipiga kunako VfB Eppingen pia amewahi kuwatumikia wekundu wa Msimbazi (Simba Sc) pamoja na timu ya taifa ya Tanzania (U20 Ngorongoro Heroes) Mugeta anayecheza ligi daraja la tano (Verbandsliga)amesema kwa sasa jambo kubwa lililoko mbele yake ni yeye kuweza kujifua zaidi ili kuweza kurudi katika kiwango chake,kabla ya Mugeta kuumia aliweza kuchaguliwa katika kikosi bora cha mwezi wa 3 kwa msimu ulioisha.

Post a Comment