SINGIDA UTD WATAJA SABABU YA KUTOKA SULUHU NA YANGA
Mara baada ya kuambulia sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Yanga hapo jana, uongozi wa Singida United umesema, mabadiliko ya wachezaji wawili ndiyo yaliyowaharibia mipango yao kwani hawakutarajia matokeo hayo.
Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema, kama isingekuwa mabadiliko ya mchezaji Shafikh Batambuze na mlinda Mlango Ally Mustapha Bartez, Yanga angekufa kwa zaidi ya goli tatu.
"Hatujutarajia kupata matokeo kama yale, tuliamini kwamba tutashinda kutokana na aina ya kikosi pamoja na maandalizi, lakini tulifanya mabadiliko kwa wachezaji wetu wawili ambao walipata majeraha lakini kwa sasa wanaendelea vizuri, " amesema.
Sanga amesema, mchezo dhidi ya Yanga ulikuwa ni maandalizi kwaajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Lipuli ambapo kikosi kinatarajia kuondoka kesho kuelekea Iringa.
Sanga amezitaka timu ambazo watakutana nazo kuondoa mawazo kwamba Singida ni ngazi ya wao kuchukulia Ubingwa au kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi.
"Kwa sasa hatupo katika mbio za Ubingwa hivyo nguvu kubwa tunazielekeza kwenye mchezo wa FA kwahiyo mara baada ya mchezo na Lipuli tutakutana na Jkt Tanzania na tunahitaji kushinda, " amesema.
"Kwenye mechi dhidi ya Simba SC ambao tutakutana nyumbani Namfua tunawaomba wajiandae kisaikolojia,wasifikiria sisi ni ngazi kwamba watakuja kupandia kwetu ili waende kuchukua Ubingwa, sisi tunacheza mpira na tunahitaji kupata matokeo mazuri kwa kila mchezo kwahiyo Simba asifikirie kwamba tutamuachia, akumbuke kwamba alishatufunga goli nne, kwahiyo hatutakubaki kufungwa tena tukiwa nyumbani, " amesema.

Post a Comment