KIMENYA AFUNGUKA KUONDOKA KWA MO RASHID, MPEPO PRISONS
Nyota wa timu ya Tanzania Prisons, Salum Kimenya amefunguka kuwa licha ya kuondoka kwa washambuliaji wao Mohammed Rashid na Eliuter Mpepo Maafande hao hawata tetereka msimu ujao.
Mo Rashid amejiunga na Simba na tayari yupo nchini Kenya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup wakati Mpepo akiwa katika hatua za mwisho kuelekea Singida United.
Kimenya ameiambia Tiktak kuwa hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya klabu, huko nyuma kuliondoka nyota wakubwa lakini Prisons imebaki hata hao wameondoka na timu ipo pale pale.
Kimenya ambaye alikuwa akitumika kama mlinzi wa kulia kabla ya kubadilishiwa majukumu na kuwa winga wa kulia amesema hakatai kuondoka kwa Maafande hao ila timu zinazohitaji saini yake zinashindwa kufikia dau analotaka.
"Prisons ni kubwa kuliko mchezaji yoyote kama Mo Rashid na Mpepo wameondoka watakuja wachezaji wengine na tutaendelea kufanya vizuri.
"Binafsi sio kama sitaki kuondoka Prisons ila timu zinazonifuata haziki kwenye dau ninalohitaji," alisema Kimenya.
Prisons ilimaliza msimu uliopita nafasi ya nne nyuma ya timu za Simba, Azam FC na Yanga.
Post a Comment