DAVID DE GEA NAYE ANATAKA KULIPWA MSHAHARA HUU NDANI YA MAN UNITED
Mshambuliaji wa Manchester United, Alexis Sanchez ndiye mchezaji
anayelipwa ghali kwenye Ligi Kuu ya England akiwa anachukua kitita cha
pauni 500,000 kwa wiki.
Sasa baada ya dili hilo kuwa linafanya kazi, kipa wa Manchester
United, David de Gea, naye yupo tayari kusaini mkataba mpya na timu hiyo
ambao utamfanya awe analipwa kitita cha pauni 375,000 kwa wiki.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuomba mkataba huo ambao utamfanya awe kipa anayelipwa ghali kwenye Ligi Kuu England.
Kipa huyo raia wa Hispania amekuwa akiwindwa mara kwa mara na Real
Madrid na Manchester wanafahamu kuwa kama hawatampa mkataba huo basi
anaweza kuondoka kwenye timu hiyo.
De Gea analipwa mshahara wa pauni 210,000 kwa wiki.

Post a Comment