MSA
Mugeta Soccer Academy(MSA)ni kituo cha kulea na kukuza vipaji
kwa vijana vile vile MSA ukiachilia mbali kukuza vipaji kwa vijana tunalojukumu
la kuwapa malezi bora vijana wetu kwa kuwapa uangalizi makini kuanzia majumbani
hadi mashuleni kwa kufuatilia maendeleo yao kitaaluma hadi kinidhamu.
MSA pia ni
kama mlezi kwani tunaona vijana ambao family zao hazina uwezo wa kuwapeleka
shule ama kuwasaidia mahitaji ya maalum shuleni hivyo MSA tunabeba jukumu hili
na kuweza kuwasaidia vijana wetu ili kuhakikisha wanafanya izuri kote kote kiwanjani
pamoja na shuleni.
Tunao
vijana wa umri mbalimbali katika kituo chetu wale wa U12,U14,U16 na
U17.Malengo yetu makubwa ni kutengeneza kizazi cha soka kitakachokuwa
tegemeo kwa taifa na bara letu.
Kituo
chetu kimeanzishwa rasmi mwaka 2016 chini ya maono ya mwanasoka wa
kitanzania anayechezea nchini ujerumani Emily Mugeta.Makao makuu ya MSA
ni wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.
No comments