ZITTO KABWE "MSIMLALAMIKIE MBWANA SAMATTA KUHUSU KWENDA KUMUONA MH TUNDU LISSU"
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amefunguka na kumtetea mshambuliaji
wa Kimataifa wa Tanzania ambaye sasa anakipiga klabu ya Genk ya nchini
Ubelgiji , Mbwana Samatta kuwa ameshinda kwenda kumtembelea Tundu Lissu
kutokana na ratiba yake kuwa ngumu.
Zitto
Kabwe aliona aweke wazi hilo kufuatia baadhi ya watu kuanza kuhoji
inakuaje mchezaji huyo yupo ameshinda japo kwenda kumtembelea na kumuona
Mbunge Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu nchini humo kufuatia
kushambuliwa kwa risasi mwaka jana. Zitto Kabwe ndipo aliamua kuweka
sawa kuwa mchezaji huyo kwa sasa ratiba yake ni ngumu lakini anaamini
atakwenda wakati ukipatiakana.
"Mbwana ni mgonjwa pia. Hivi sasa yupo kwenye mazoezi chini ya ratiba ngumu Sana ili arudi hali yake ya kawaida. Mjue kuwa Mbwana ni profeshno hawezi kwenda kinyume na ratiba ya daktari kama huko kwetu. Msimwingize kwenye haya mambo tafadhali. Atamwona Lissu kwa wakati wake" aliandika Zitto Kabwe
Zitto Kabwe kwa sasa yupo nchini Ubelgiji ambapo alipata nafasi ya kumtembelea Mbunge Tundu Lissu anapopatiwa matibabu pia aliweza kumtembelea mchezaji huyo wa Genk

Post a Comment