BENCHI LA UFUNDI NGORONGORO HEROES LAANZA MAANDALIZI YA AFCON 2019
Kuelekea katika maandalizi ya Michuano ya AFCON ya vijana
wenyeumri chini ya Miaka 20, benchi la ufundi la timu ya Ngorongoro
Heroes limeanza maandalizi kwaajili ya mchezo wa kwanza dhidi ya DR
Congo utakaochezwa Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Akizungumza wakati wa kutaja kikosi hicho, Kocha msaidizi wa Ngorongoro Heroes Oscar Milambo amesema, vijana hao wameshaingia kambini tangu Machi 06 mwaka huu huku wakitarajia kufanya mchujo Machi 11 kwaajili ya kupata kikosi kamili cha wachezaji 30 kitakachoendelea na maandalizi ya kuwania kufuzu kushiriki fainali za AFCON zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.
“Tuajukumu kama Taifa ambalo lipo mbele yetu la kwenda kwenye michuano ya kuwania kushiriki AFCON kwa vijana wa Ngorongoro Heroes ambao ni U20 na tayari ratiba tunayo kwamba mchezo wa kwanza Tanzania tumepangwa kucheza na DR Congo Machi 31 ambapo marudiano utakuwa Aprili 21 lakini pia kama tukifanikiwa kuwafunga Congo mzunguko wa pili tutakwenda kucheza na Mali Mwezi Mei na tukifanikiwa hapo tutakwenda kucheza na mshindi kati ya Cameroon na Uganda Mwezi Julai, ” amesema.
Kocha Milambo amesema, Kikosi hicho kinaundwa na vijana wote waliokuwa Serengeti Boys walioshiriki mashindano ya AFCON 2017 kama uti wa mgongo lakini kama taratibu za CAF wameruhusiwa kutumia wachezaji waliozaliwa kuanzia Januari Mosi 1999 na kuendelea.
Kikosi cha Serengeti Boys mwaka 2017 ambapo mwaka huu ndio wanaunda Ngorongoro Heroes
Kwaujumla wachezaji walioitwa kuunda Kikosi hicho ni:

- Ramadhan Kabwili - Yanga
- Kibwana Ally Shomary (Mtibwa Sugar)
- Ally Msengi - (Mbao)
- Enrick Vitalis Nkosi (African Lyon)
- Dickson Nickson Job (Mtibwa Sugar)
- Assad Ally Juma (Singida United)
- Said Mussa Bakary (Yanga)
- Ally Hamis Ng'anzi (Singida United)
- Kelvin Nashon Naftal (JKT Tanzania)
- Shaaban Zubari Ada (Lipuli FC)
- Isa Abdi Makamba (Singida United)
- Mohamed Abdallah Rashid (Singida United)
- Marco Gerard (JMK)
- Syprian Benedictor Mtesigwa (Toto Africa)
- Muhsin Malima Makame (Njombe Mji)
- Yohana Oscar Mkomola (Yanga)
- Ibrahim Abdallah (Miembeni City)
- Abdul Hamis Suleiman (Ndanda FC)
- Nickson Clement Kibabage (Njombe Mji)
- Mussa Mussa Najimu (Changanyikeni)
- Maziku Amede Aman (Makongo)
- Hamis Mustafa (Ndanda FC)
- Abutwalib Mshed (Mtibwa Sugar)
- Samson Peter Myati (Toto Africa)
- Said Issa Mohamed (Azam FC)
- Ayoub Mohamed (Yanga)
- Mohamed Mussa (Azam FC)
- Emmanuel Mnyati (Tanzania Prisons)
- Riffat Hamis (Mtibwa Sugar)
- Oscar Masai (Azam FC)
- Johnny Kwiyenda (Makongo)
- Paul Peter (Azam FC)
- Ally Salimu (Simba SC)
- Vitalis Mayanga (Africa Lyon)
- Rajab Odas Mohamed (Azam FC)
- Pontia Frank Ohonya
- Makka Antony (Yanga)
- Israel Ptrick Mwenda (Alliance)
- Hance Masoud Msonya (Alliance)
- Mosses Kitandu (Simba SC)
- Ibrahim Ally (Azam FC)
Post a Comment