HATIMAYE NAOMI OSAKA AMETWAA UBINGWA WA MICHUANO HII YA TENNIS.
Mwanadada raia wa Japani, Naomi Osaka kwa mara yake ya kwanza tangua kuanza mchezo wa tennis amefanikiwa kutwaa taji kubwa la michuano ya wazi la BNP Paribas au WTA Indian Wells baada ya kumshinda Daria Kasatkina.
Osaka amelitwaa taji hilo Jumapili hii kwa kumfunga Daria Kasatkina kwa jumla ya seti 6-3 6-2.
Mara baada ya ushindi huo, Osaka ameviambia vyombo vya habari kuwa lengo lake lilikuwa ni kutwaa taji hilo.
Nilikuwa na hofu kubwa lakini nikajiamini na kusema malengo yangu ni kutwaa ubingwa.
Nilijua mpinzani wangu atapambana kwa kila pointi hivyo siku na sababu ya kupoteza nilihakikisha nafanya vizuri na kufanya maamuzi yaliyo sahihi.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.


Post a Comment