KATWILA: TUTAFANYA USAJILI 'BAB KUBWA' MSIMU UJAO


Baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya Azam Sports Federation Cup timu ya Mtibwa Sugar imejipanga kufanya usajili mkubwa kwa ajili ya michuano ya kombe Shirikisho Afrika mwakani.

Mtibwa wametawazwa mabingwa wa michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi Singida United katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Katwila amesema lazima wafanye usajili mkubwa kwa ajili ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika mwakani na tayari ameshaona mapungufu yaliyopo.

"Lazima tufanye usajili mkubwa kwa ajili ya michuano ya Shirikisho, tunahitaji kukiongezea nguvu kikosi chetu ingawa kipo imara. Itanibidi niongezee nyota wengine ili tusionekane tunasindikiza wengine," alisema Katwila.

Mtibwa imekuwa haina utamaduni wa kusajili wachezaji wa kigeni kutoka nje wakiamini zaidi vijana kitu ambacho kinasubiriwa kuonekana kama wataendelea na utaratibu huo au watavuka mipaka ya nchi kusaka majembe.

No comments