SIMBA YAJIFUNZA KWA YANGA, YAAHIDI KURUDI NA TAJI DAR
Baada ya Yanga kutolewa kwenye michuano ya SportPesa Super Cup watani wao wa jadi Simba wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri ili kurejea na taji hilo nyumbani.
Simba itatupa karata yake ya kwanza katika michuano hiyo leo saa 9 alasiri dhidi ya Kariobangi Sharks na ikishinda itaingia nusu fainali.
Meneja wa Simba, Richard Robert amesema wamejifunza kwa kilicho wakuta Yanga kwahiyo wataingia kwa tahadhari kubwa wakishusha kikosi kizima.
"Tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri na lengo letu nikurejea Dar es Salaam na taji hili la SportPesa.
"Wenzetu Yanga jana wametolewa na sisi hatutaki aibu hii itukute tumejipanga kufanya vizuri tukianza na mechi ya leo," alisema Richard.
Bingwa wa michuano hiyo atasafiri kwenda Uingereza kucheza na timu ya Everton katika uwanja wa Godson Park.

Post a Comment