BD YATAJA SIRI YA USHINDANI LIGI YA MKOA WA DAR ES SALAAM

Chama cha Mpira wa kikapu Mkoa wa Dar es salaam (BD) kimesema ushindani wa Ligi ya Mkoa kwa msimu huu umeongezeka kutokana na kila timu kuwa na maandalizi mazuri ikiwemo usajili kwa wachezaji huku kikivitaka pia vilabu kufuata kanuni na sheria zilizopo.

Mkurugenzi wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam Misoji Mihayo amesema, kwa mwaka huu wanaamini watakuwa na Ligi yenye ushindani ambayo itasaidia pia kupata hata wachezaji wazuri watakaounda Timu ya Taifa.

“Hali ya ushindani kwa Ligi ya Mkoa imekuwa tofauti na mwaka jana, mwaka huu Ligi imekuwa ni ngumu sana hata ukiangalia timu ambazo zimepanda daraja zinaonyesha ushindani mkubwa na wahali ya juu, lakini vilevile uskizingatia timu zimefanya usajili mkubwa kama timu za Oilers, Pazi, JKT na kuna vijana wamepandishwa kutoka timu ya pili kwahiyo hii inaonyesha kabisa kwamba Ligi itakuwa ni ngumu sana kwa msimu huu, ” amesema.

Mihayo amesema, kumekuwa na changmoto kwa baadhi ya Timu kushindwa kusoma kanuni kwa umakini hivyo kupelekea kufanya makosa ndani ya Ligi hiyo lakini kwa upande wao wakiwa ndio waandaaji na wasimamizi wa Ligi hiyo watahakikisha wanasimamia sheria ili kuhakikisha wanaweka hali ya usalama katika Ligi hiyo.

“Masuala ya waamuazi bado kunabaadhi ya vilabu vinalalamikia waamuzi lakini suala ni kwamba vilabu visome kanuni ambazo tumejiwekea wenyewe, kama ambavyo tumeona juzi kwa Kocha mkubwa tuu wa Timu ya vijana amefanya fujo kwenye benchi, kwa hiyo sisi tukiwa ndio chama tutafuata kanuni zetu na sheria zitafuata mkondo wake kwa kila atakayefanya kosa ataadhibiwa kwa mujibu wa katiba, sheria na kanuni tulizojiwekea, ” amesema.

Mihayo ameongeza kuwa kwa upande wa udhamini wapo katika mazungumzo mazuri na moja ya kampuni ambayo wanaaminimpaka kufikia Aprili mwaka huu tayari watakuwa na wadhamini.



No comments