TSA YAANDAA MASHINDANO YA MASTERS YA MCHEZO WA KUOGELEA YATAKAYOFANYIKA MACHI 03 JIJINI ARUSHA

Mashindano ya mchezo wa kuogelea yanayofahamika kama Masters yanatarajia kufanyika Aprili 03 mwaka huu Jijini Arusha kwa kushirikisha waogeleaji wenye umri kati ya miaka 25 mpaka 99.

Katibu mkuu wa chama cha mchezo wa kuogelea nchini (TSA) Ramadhan Namkoveka amesema, hakuna nchi yoyote alikwa katika mashindano hayo yenye lengo la kukuza mchezo huo pamoja na kupata timu itakayoshiriki mashindano ya Kimataifa ya Masters yatakayofanyika mwaka huu nchini Afrika Kusini.

“TSA tutakuwa na mashindano ya Masters, mashindano haya yanahusisha waogeleaji kuanzia umri wa miaka 25 mpaka 99, lengo ni kuweza kuinua na kuuendeleza mchezo huu wa kuogelea hapa nchini, tukumbuke kwamba mwanzoni kabisa mwa Januari tulikuwa na kozi ya waamuzi, pia tukawa na mashindano ya vijana na sasa hivi tunaangalia Masters, ” amesema.

Namkoveka amewataka waogeleaji kujitokeza kwaajili ya kuhakiki ushiriki wa mashindano hayo ambayo yatakuwa chini ya Arusha Swimming Club huku akiongeza kuwa iwapo hawatashiriki mashindano ya Kimataifa ya Afrika Kusini wataangalia nafasi itakayopatikana kwaajili ya kuweza kushiriki amoja na kuyaendeleza mashindano hayo.

No comments