HATUTAKUBALI KURUDIA MAKOSA KATIKA MCHEZO WA KESHO DHIDI YA YANGA, TUNAHITAJI SARE AU USHINDI - UONGOZI NA WACHEZAJI WA MAJIMAJI FC


Kuelekea katika mchezo wa kesho utakaowakutanisha Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Yanga dhidi ya Majimaji ya Songea Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Kikosi cha Majimaji FC kimesema hakitakubali kurudia makosa ambayo yalichangia kupoteza mchezo dhidi ya Simba SC ikiwa ni muendelezo wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara mzunguko wa lala salama.

Afisa habari wa Klabu ya Majimaji Onesmo Ndunguru amesema, kikosi kipo imara japo kitawakosa wachezaji wake wawili ambao ni majeruhi lakini kimejipanga kwaajili ya kuweza kubeba pointi tatu au hata sare ili kuweza kujitengenezea nafasi nzuri katika mzimamo wa Ligi.

Kikosi kipo tayari kupambana na kocha ameshafanya marekebisho kwa makosa yaliyokuwa yakijitokeza ambapo eneo kubwa ni katika safu ya ushambuliaji kwani timu imekuwa ikitengeneza bafasi nyingi lakini imekuwa haipati magoli hivyo amekamilisha kurekebisha na leo tumeshafanya mazoezi ya mwisho asubuhi kwaajili ya mchezo wa kesho ambao tunaamini tutapambana kupata pointi tatu muhimu au sare, ” amesema.

Ndunguru amesema wachezaji takribani 20 walionao kambini wapo tayari kwaajili ya kuweza kutimiza maagizo ya kocha isipokuwa wachezaji wawili ambao wamewaacha Mjini Songea kwaajili ya matibabu ambao ni Beki Juma Abdallah Salamba na Idrissa Mohamed.

Kwaupande wake Nahodha wa Kikosi hicho Hamis Hassan amesema, wamepokea maelekezo ya Kocha ambayo wanaamini yatawapa mwangaza wa kuibuka na ushindi huku Marcel Boniventure ambaye ni mshambuliaji ndani ya kikosi hicho akiwataka mashabiki kutokukata tamaa kwani wapo tayari kwaajili ya kuhakikisha timu inashinda katika kila mchezo uliombele yao.

Tupo tayari kwaajili ya mchezo wa kesho, maandalizi tuliyaanzia nyumbani na kama tunavyojua Ligi ni ngumu lakini tutajitahidi kwaajili ya kupata pointi ambazo zitatuweka katika nafasi nzuri katika Ligi, ” amesema Nahodha wa Majmaji FC, Hamis Hassan.

Mzunguko wa pili ni mgumu kwani kila timu inapambana kuhakikisha inakuwa katika nafasi nzuri lakini sisi pia tumejipanga kwaajili ya kuhakikisha tunapambana, mchezo dhidi ya Simba SC tunakiri tulipoteza kwakuwa hatukufuata maelekezo ya kocha lakini katika mchezo wa kesho tunaamini kwa maelekezo ya kocha tutafanya vizuri, ” amesema Mshambuliaji wa Majimaji FC, Marcel Boniventure.

  KIKOSI CHA MAJIMAJI

                                                        

No comments