WANAWAKE SAUDI ARABIA WAMEINGIA KWA MARA YA KWANZA UWANJANI
Hatimaye wanawake nchini Saudi Arabia wameingia kwa mara ya kwanza
kwenye viwanja vya mpira kushuhudia mchezo huo pendwa zaidi duniani.
Wanawake hao waliohudhuria kwenye mchezo wa Derby ya Ryadh kati ya
Al-Nassir FC na Al-Hilal FC kwenye Uwanja wa Taifa wa King Fahad
wikiendi iliyopita walionekana wenye furaha huku wengi wakiimba kuwa
wamekombolewa na wamekuwa binadamu wa kawaida kama wanawake wengine
duniani.
Wanawake hao ambao waliongozwa na mwanaharakati Madeha al Ajroush
(63) ambaye ndiye amekuwa akipigania haki za wanawake kuingia viwanjani
na kuendesha magari tangu akiwa na miaka 18, amesema ni furaha kuona
malengo yake yamekamilika ingawaje umri umemtupa mkono.
“Tangu nikiwa na miaka 18 nilijua itafika muda wanawake
tutaendesha magari na kuingia kwenye viwanja na kweli imetimia ingawaje
hatua imechelewa hadi sasa nina miaka 63 lakini imenipa funzo katika
maisha yangu,“amesema Bi. Al Ajroush ambaye amefungwa zaidi ya mara tatu akipigania usawa wa kijinsia nchini Saudi Arabia.
Wanawake wengine walioonekana uwanjani hapo walisikika wakiimba na
kushangilia kwa furaha sio kwa sababu ya mpira bali kutokana na
kuruhusiwa kuingia viwanjani.
“Tunajiona kama tumekuwa binadamu kwa sasa kwani tunaweza
kujiamulia kipi cha kufanya na sio kuamuliwa na mtu kama ilivyo kuwa
awali,“amesikika Mwanafunzi wa kike wa miaka 18 kwenye mahojiano na Sky News.
Hatua hiyo imekuja baada ya baada ya mwaka jana nchi hiyo kuruhusu
wanawake kuendesha magari na kuanza kuingia viwanjani kuanzia mwaka huu.
Awali wanawake nchini humo walikuwa hawaruhusiwi kuingia viwanjani
lakini kuanzia mwaka huu wataingia kwenye viwanja vya michezo kwa
masharti ya kujifunga Hijab na Niqab.



Post a Comment