MOTO WA SIMBA KUWASHWA LEO KAZI WANAYO GENDERMARIE KUTOKA DJIBOUT.

Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba baada ya kukaa nje ya mashindano ya kimataifa kwa miaka mitano leo wataonyesha makali yao dhidi ya Gendermarie ya Djibout.


Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre atawaanzisha washambuliaji wake mahiri, John Bocco na Emmanuel Okwi katika safu yake ya ushambuliji katika kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa nyumbani.
 
Okwi na Bocco kwa pamoja wamefunga mabao 22 katika Ligi Kuu na kasi hiyo na uzoefu wao katika mashindano ya kimataifa unaipa Simba nafasi kubwa ya kushinda mechi hiyo.
 
Okwi alisema "Msimu huu tuna uongozi mzuri unatupa hamasa ya kufanya vizuri kila mechi. Pia wachezaji vijana wengi wana morali ya kupata mafanikio, kwahiyo tunaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kutushangilia ili tuweze kushinda."
 
Kocha msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Djuma alisema mechi haitakuwa rahisi kushinda, lakini wamejipanga kuweka hesabu zao sawa kabla ya mechi ya marudiano itakayochezwa siku 10 baadaye.
 
Djuma alisema Gendarmerie ina safu nzuri ya ulinzi na maandalizi waliyofanya kuelekea kwenyee Nchi hiyo ni kutengeneza mbinu za kupenya kirahisi.

"Ukishindwa kufanya vizuri nyumbani, ugenini mzigo unakuwa mkubwa na ni mara chache unaweza kupata matokeo mazuri hivyo tumejipanga kuhakikisha tunatumia mapungufu yao ili kuwafunga," alisema Djouma.

No comments