USHINDI HUU WA SIMBA UMELETA MATUMAINI KWA WATANZANIA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
Klabu ya Simba huenda ikawatoa kimasomaso Watanzania kwenye michuano
mikubwa barani Afrika ya Kombe la Shirikisho kutokana na ushindi mnono
wa leo wa goli 4-0 dhidi ya klabu ya Gendamarie Tnale kutoka nchini
Djibouti.
Magoli ya Simba yamefungwa na John Bocco 33′, 44′ , Emannuel Okwi 90+ na Said Ndemla kunako dakika ya 2 ya mchezo.
Kwa ushindi huo hakuna shaka kuwa Simba watafanikiwa kusonga mbele
kwenye mchezo wa marudiano hii ni kwa jinsi kikosi cha Gendamarie Tnale
kilivyo hakitakuwa na uwezo wa kumtwanga mnyama goli 5-0 ili kusonga
mbele ingawaje mpira haupo hivyo ila Simba wameonesha matumaini kwa
Watanzania.
Hayo yamejiri wakati ambapo mahasimu wao Klabu ya Yanga jana wamepata
ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya St Louis mchezo wa klabu
bingwa Afrika raundi ya kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.

Post a Comment