MWAKYEMBE AZIKURUPUA YANGA NA SIMBA KUHAKIKISHA WANALIFANYA HILI IPASAVYO.
Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na
Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amezishangaa timu za Yanga na Simba za
Tanzania kuwa licha ya umri mrefu lakini hazina viwanja vyao vya
michezo.
Dk Mwakyembe ametoa kauli hiyo bungeni
wakati anajibu mwongozo wa mbunge wa Mchinga Hamidu Bobale kuhusu timu
ya Yanga kuwaachia uwanja timu ya St Louis ya kutoka Shelisheli.
"Yanga wana miaka 83 tangu kuanzishwa
kwake na Simba wana miaka 82, ni wakati wa kujitafakari kwani zisiwe na
viwanja vyao sasa," amehoji Mwakyembe.
Akizungumzia Uwanja wa Taifa amesema
uwanja huo una masharti ambapo hautakiwi kuzidisha michezo mitatu kwa
wiki ili uweze kudumu walau miaka kumi tangu matengenezo yake.
Hata hivyo alisema inamshangaza na bado
anakuwa na mashaka na watendaji wake kwa kuruhusu michezo mingi ambapo
kwa wiki hii uwanja utakuwa umetumika mara tano kitu alichokiita ni
Uswahili'.
Mwakyembe amesema mchezo wa Yanga na St Louis kwa kesho itafuatia mechi ya Simba keshokutwa zote zikitumia uwanja huo.
Bobale alisema timu za Tanzania huwa
zinafanyiwa mtimanyongo ziwapo nje ya nchi na kuhoji zababu za TFF
kuwapa uwanja wageni ambacho alisema ni hujuma kwa Yanga.
Waziri alipinga hoja hiyo akisema siyo nzuri katika mahusiano na kwamba wanatakiwa kupewa uwanja ili waanze kuuzoea.

Post a Comment