KYRIE IRVING AKUMBWA NA MKOSI, GIANNIS ANTENTOKOUNMPO MCHEZAJI BORA NBA?

Inawezekana jina la Giannis Antetokounmpo
likawa maarufu kutokana na ugumu wake lakini tangu msimu uliopita
amekuwa mchezaji anayetizamwa zaidi katika kundi la wachezaji vijana
wanaoweza kuja kuitikisa NBA. Hii ndio sababu ambayo Kevin Durant
alikiri kuwa Giannis ni mchezaji wa kipekee na anaweza kumaliza maisha
ya NBA akiwa mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea.
Alfajiri
ya Leo, Giannis aliiongoza klabu yake ya Milwaukee Bucks kushinda
mchezo wao wa kwanza dhidi ya Boston Celtics ambayo sasa itakuwa
imepoteza michezo miwili mfululizo. Boston Celtics ambayo inaonekana
kuwa na kikosi kipya kabisa kilichojaa vijana baada ya kuondokewa na
nyota wake kama Isaiah Thomas, Avery Bradley, Jae Crowder na Kelly
Olynyk imepoteza mchezo wake wa ili mfululizo huku ikiwa ni siku moja
tangu kumpoteza nyota wao Gordon Hayward aliyevunjika vibaya dhidi ya
Cleveland Cavaliers.
Giannis Antentokounmpo alifunga pointi 37 huku pia akidaka rebound 13, huku wenzie Malcolm Brogdon akifunga pointi 19 na Khris Middleton akiongeza pointi 15 na kudaka rebounds 9 lakini pia Mathew Dellavedova alitoa mchango wake wa pointi 15 kwenye ushindi huo.
Kyrie Irving
alikuwa na usiku atakaotaka kuusahau baada ya kumaliza mchezo na pointi
17 huku akipata mitupo 7 tu kati ya 25 aliyojaribu ikiwa ni mchezo wake
wa kwanza nyumbani kwa Boston Celtics yaani TD Garden, Jaylen Brown yeye aliongeza 18.
Kabla ya mchezo huo, kwenye screen maalumu ndani ya uwanja wa TD
Garden, ilipita video ikimuonyesha Gordon akiwa hospitali akiwashukuru
washabiki na wachezaji wenzie kwa kumtakia heri katika kuuguza majeraha.
Post a Comment