SIMBA KUONDOKA LEO KWA AJILI YA MCHEZO WA MAREJEANO DHIDI YA GENDERMERIE YA DJIBOUTI.

Klabu ya soka ya Simba imethibitisha kuondoka   leo kuelekea nchini Djibouti kwaajili ya mchezo wake wa marejeano dhidi ya wenyeji wao Gendarmerie kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. 


Kupitia kwa taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano ya klabu hiyo imeeleza kuwa kikosi cha Simba kilifanya mazoezi ya mwisho jioni ya jana tayari kwa safari ya kwenda kusaka tiketi ya kutinga hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Simba ambayo ilishinda mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam inahitaji sare tu au isifungwe zaidi ya mabao manne ili kuvuka hatua hiyo ya awali ya michuano hiyo.

Kikosi cha Simba ambao ndio vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara kitaondoka nchini majira ya saa 11:00 jioni siku ya leo ambapo mchezo wao unatarajiwa kupigwa Februari 21.
Aidha simba  inaelekea katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Mwadui Fc katika ligi kuu soka Tanzania Bara.

No comments