MOURINHO AMETOA SABABU YA POGBA KUONDOLEWA KIKOSINI SIKU YA JANA
Nyota wa Manchester United Paul Pogba ameondolewa kwenye kikosi cha timu
hiyo kitakachoivaa Huddersfield kwenye mchezo wa FA raundi ya 16 baadae
usiku wa leo.
Kocha
Jose Mourinho amesema alimjumuisha Pogba kwenye kikosi lakini
amelazimika kumwondoa kutokana na kuumwa ghafla japo hajaweka wazi ni
ugonjwa gani umempata nyota huyo wa Ufaransa.
Baada ya kuondolewa kikosini nafasi ya Pogba imechukuliwa na kinda Ethan Hamilton mwenye umri wa miaka 19 kutoka timu ya vijana ya Manchester United.
Katika mchezo huo wa leo Manchester United itakuwa ugenini kwenye uwanja wa Kirklees, ambapo itakuwa inasaka nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Hata hivyo Mourinho hajasema kama ugonjwa aliopata Pogba unawezekana ukathiri nafasi yake kwenye mechi ya UEFA dhidi ya Sevilla kwenye uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan Jumatano ijayo.

Post a Comment