Simba na Yanga kula viporo kabla ya safari
Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC iliyopo kileleni mwa
msimamo na mabingwa watetezi Yanga SC iliyopo nafasi ya pili
zinatarajiwa kucheza mechi zao za viporo za VPL kabla ya kusafiri kwa
mechi za kimataifa.
Yanga ambayo haikucheza mchezo wake wa raundi ya 18 kutokana na
wikiendi ililiyopita kucheza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika
dhidi ya St. Lousi ya Shelisheli, itaikaribisha Majimaji FC kwenye
uwanja wa Uhuru.
Simba wao hawakucheza mchezo wao wa raundi ya 18 kutokana na
kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika
ambapo walicheza na Gendarmerie ya Djibouti. Alhamisi watakuwa mjini
Shinyanga kucheza na Mwadui FC.
Tayari Yanga wameshaweka wazi kuwa watasafiri siku ya Jumapili
Februari 18 kuelekea Shelisheli kwaajili ya mchezo wa marudiano
utakaopigwa Februari 21. Simba bado hawajatangaza lini wataondoka
nchini.
Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 41 huku wapinzani wao wa
Alhamisi Mwadui wakiwa katika nafasi ya 12 na alama 18. Yanga ina alama
34 katika nafasi ya tatu huku Majimaji wakiwa nafasi ya 14 na alama 14.

Post a Comment