ORODHA YA VIKOSI GHALI ZAIDI DUNIANI IMETOKA NAFASI YA ARSENAL NA REAL MADRID HII HAPA.
Kwenye orodha hiyo ya timu 50 iliyotolewa na Taasisi ya CIES Football Observatory imeonesha kuwa timu kutoka Uingereza zimeongoza kwenye 10 bora.
Kwenye nafasi ya kwanza kwenye orodha hiyo Man City imeongoza ambapo
kikosi chake kina gharama ya Euro milioni £777 ikifuatiwa na vikosi vya
PSG Euro Milioni £713, Man United Euro milioni £661 na FC Barcelona
Euro milioni £641
Katika hali ya kushangaza ni kwamba timu ambazo zinatajwa kuwa na
mkwanja mrefu duniani za Real Madrid, Bayern Munich na Arsenal hazipo
kwenye Tano bora ya klabu zenye vikosi ghali duniani licha ya kuingiza
faida kubwa kwenye dili za matangazo, mikataba na makampuni na mauzo ya
jezi.
Kwenye orodha ya vikosi ghali kwenye 10 bora Uingereza imetoa timu
sita ikifuatiwa na Hispania timu mbili huku Italia na Ufaransa zikitoa
timu moja moja.
Tazama orodha kamili ya timu 50 zenye vikosi ghali zaidi duniani kwa msimu huu 2017/18.

Post a Comment