WACHEZAJI SINGIDA UNITED WAZIVAA ADHABU ZA TFF MECHI YA FA DHIDI YA GREEN WORRIOURS
Kamati
ya mashindano ya Shirikisho la Soka nchini TFF imewafungia mechi tatu
za Kombe la Shirikisho (FA) Mshambuliaji wa Singida United Deus
Kaseke na Mlinda Mlango wa Green Warriors Shaaban Dihile pamoja na
faini ya Shilingi laki Tano kila mmoja huku Kambale Salita “Papy
Kambale” wa Singida naye akipelekwa kwenye kamati ya Nidhamu.
Mkurugenzi
wa Mashindano wa TFF Efrem August amesema, Kamati ilikutana Februari
13 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine ilipitia taarifa za
mchezo huo ambapo ilionyesha kuwa Kaseke na Dihile hawakuingia
uwanjani na timu zao na hawakuwepo wakati timu hizo zikipeana mikono
Uwanjani.
“Wachezaji
Deus Kaseke na Shaaban Dihile wamefungiwa mechi tatu pamoja na faini
ikiwa ni kwamujibu wa kanuni za Kombe la Shirikisho Kanuni 31 kifungu
cha kwanza ambayo inaelezea kwamba kwa kosa hilo wachezaji waadhibiwe
kulingana na kanuni ya Ligi husika ambapo tukienda kwenye kanuni ya
Ligi kuu ambapo Singida wanashiriki, kanuni namba 37 kifungu cha 7 D
kinaelekeza kwamba mchezaji afungiwe mechi tatu na Faini ya Shilingi
Laki 5, kwahiyo hawatashiriki mechi tatu za Kombe la Shirikisho, ”
amesema.
Efrem
ameongeza kuwa, Papy Kambale aamepelekwa kwenye kamati ya Nidhamu ay
TFF kwa kosa la kumpiga mchezaji wa timu pinzani kwenye mchezo
uliozikutanisha timu hizo Januari 31mwaka huu Uwanja wa Azam Complex
Chamazi ambapo kamati ya Nidhamu ya TFF itatoa maamuzi zaidi kuhusu
kosa lake.
| Wachezaji wa Singida United
Mudathir Yanya na Deus Kaseke
|
Post a Comment