ARSENAL WAENDELEZA UBABE EUROPA LEAGUE DOTMOND WAOKOLEWA NA WASHAMBULIZI WA CHELSEA.
Usiku wa kuamkia leo michezo 16 ya kombe la Uefa Europa League imechezwa
katika hatua ya timu 32 bora. Miongoni mwa mechi zilizochezwa ni
Ostersunds ya Sweden dhidi ya Arsenal ambao wlikuwa wageni wa mchezo
huo.
Katika mchezo huo Arsenal walipata ushindi wa mabao 3-0. Mabao hayo
yalifungwa na Nacho Monreal dakika ya 13, Mesut Ozil 58 na bao la
kujifunga la Sotirios Papagiannopoulos kwenye dakika ya 24.
Katika mchezo mwingine uliochezwa Borussia Dortmund ambao walikuwa
nyumbani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3 dhidi ya mawili ya
Atalanta. Mabao ya Dortmund yalifungwa na wachezaji wa zamani wa
Chelsea, André Schürrle dakika ya 30 na Michy Batshuayi sliyefunga mara
mbili, katika dakika ya 65 na 90.
Nao Atalanta walipata mabao yao yote mawili kupitia kwa Josip Iličić,
akika ya 51 na 56. Haya hapa chini ni matokeo ya mechi nyingine.



Post a Comment