BD YAAHIRISHA MECHI ZA LIGI ILI KUOMBOLEZA KIFO CHA MCHEZAJI ALIYEFARIKI GAFLA
Chama cha Mpira wa KikapuMkoa wa Dar es salaam (BD) kimeahirisha michezo ya Ligi ya mkoa wa Dar es salaam (RBA LEAGUE) iliyokuwa ichezwe wiki hii kutokana na kifo cha Mchezaji
wa kikapu wa timu ya JKT Yvonne Christopher Wambura aliyefariki gafla jana.
Shirikisho limesema, kwa mujibu wa Kanuni za Shindano 2018 kifungu cha 4 (b) Kinapotokea Kifo cha Mchezaji aliyesajiliwa katika Msimu husika wa Shindano
1. Michezo yote ya Timu za JKT iliyokuwa ichezwe Leo na siku ya Jumapili Inaahirishwa ili Kupata muda wa Kutosha kushughulika na Msiba
Michezo hiyo itapangwa siku nyingine
2.Michezo ya RBA/Ratiba ya siku za ijumaa Tar 23 March 2018 Itabaki Kama ilivyo
3.Ratiba Michezo yote ya Siku J'mosi itaahirishwa Kupata Muda kwa wana Kikapu wote kuhudhuria Maziko.
3. Mabadiliko ya Muda wa michezo J'Pili Tar 25 March 2018
External heroes/Oysterbay 1000hrs
Udsm Outsider /Srelio 1200hrs
Pazi/Kigamboni 1400hrs
Vijana/Mabibo 1600hrs
Jogoo/Magnet 1800hrs
Yvonne anatarajiwa kuagwa siku ya Jumamosi Kikosi cha JKT kabla ya mazishi ambayo yatafanyika jijini Dar es salaam.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Mpendwa wetu Ivonne Mahala pema Peponi
![]()
| |

Post a Comment