JMK PARK KUANZA AWAMU MPYA YA KUKUZA VIPAJI VYA VIJANA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA
Vijana takribani 30 wakiume na wa kike wanatarajia kuanza mafunzo
ya Mpira wa kikapu mwanzoni mwa wiki ijayo katika kituo cha
michezo kwa vijana, JMK Park jijini Dar es Salaam lengo
likiwa ni kupata wachezaji bora wa hapo baadae.
Kocha wa Mpira wa Kikapu kwa vijana ambaye pia ni Mratibu wa programu za mchezo wa kikapu kwa vijana hapa nchini, Bahati Mgunda amesema, vjana hao wameptokana na mchujo walioufanya huku wakiwa na changamoto ya kupata watoto wa kike.
“Kupata watoto wakike imekuwa changamoto na hii inatokana na malezi japo tumekuwa na juhudi za kuwaelimisha wazazi na tunaendelea vizuri japo tunahitaji kuongeza juhudi kuelimisha wazazi kuhusu michezo kwa watoto wote wakike na wakiume, ” amesema.
Kocha Bahati amesema, Mafunzo hayo kwa vijana yatakuwa chini ya Makocha waliokatika kituo hicho na wanaamini wataweza kutimiza malengo yao waliyojiwekea katika kukuza vipaji vya vijana katika mpira wa kikapu.
Kocha Bahati amesema kuwa programu hiyo imesaidia katika kupata wachezaji ambao wataendelea kuboresha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 ambao wamefanya vizuri katika misimu iliyopita lakini pia wamefanikiwa kutoa wachezaji ambao wapo nje ya Tanzania wakiendeleza vipaji vyao pamoja na masomo.
“Kikubwa zaidi ambacho tumeweza kukifanya ni kwamba mwaka jana kupitia kituo chetu tuliweza kutoa vijana sita ambao waliitwa kwenda kwenye Kambi inayofahamika kama ya Giant of Afrika Camp ambayo ilifanyika Jijini Nairobi nchini Kenya na waliweza kufanya vizuri na tunatarajia mwakani hiyo Kambi itakuja hapa Nchini lakini kingine ambacho unaweza ukawa hukioni au unakiona ni kwamba wachezaji wengi tunatarajia watakuwa kwenye timu ya Taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 18 na pia ni kama nusu ya wachezaji walicheza kwenye Timu ya taifa ya chini ya miaka 16, ” amesema.
Kocha Bahati amesema, pia wametoa mchango wa vijana katika Ligi ya Mkoa wa Dar es salaam inayoendelea ambapo wachezaji wengi waliokuwa katika kituo cha kukuza vipaji wapo katika Timu mbalimbali shiriki.

Post a Comment