IFAHAMU SABABU YA KOCHA MAYANGA KUWAACHA JOHN BOCCO, THOMAS ULIMWENGU, NA HAMIS ABDALLAH KWENYE KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA STARS.
Kikosi cha wachezaji 14 wa Timu ya Taifa ya Tanzania"Taifa Stars" kimeondoka hii leo kuelekea nchini Algeria ambapo kitaungana na wachezaji wengine saba wakiwemo wa Simba pamoja na wale wa Kimataifa ambao wameshatangulia nchini humo na kufanya jumla ya wachezaji 21 kwaajili ya mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya wenyeji wao Algeria utakaopigwa Machi 22 Mwaka huu.
![]() |
| Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania salum mayanga |
Kocha wa Taifa Stars Salum Mayanga amesema, katika kikosi hicho yamefanyika mabadiliko madogo kwa wachezaji ambao wameshindwa kujiunga na kikosi kutokana na kuwa majeruhi pamoja na kukosa vibali aliwemo John Bocco, Farid Mussa, Thomas Ulimwengu na Hamis Abdallah huku akiwaongeza Himid Mao, Shaaban Iddy na Rashid Mandawa huku Kocha akielezea umuhimu wa mechi zote za kirafiki walizozipata kwa kipindi hiki.
"Wachezaji wameanza kuingia kambini jana na wengine wameingia kambini jana na hapa tunaondoka na wachezaji 14 na wachezaji saba tutakutana nao kule wakiwemo wa simba na wale wakimataifa, " amesema.
Mayanga amesema muda mrefu wamekuwa wakihitaji mechi za aina hii hivyo wanaamini zitawasaidia kuonyesha uwezo wa wachezaji kabla ya kuanza mechi za kuwania kufuzu kwa AFCON.
"Ni mechi nzuri kwetu kwasababu mechi zinazofuata za kuwania kufuzu AFCON tunacheza na Cape Verde mechi mbili hivyo zitatusaidia kujua uwezo wa wachezaji kabla, na hata kuongeza kujiamini kwa wachezaji wetu, " amesema.
Mayanga ameongeza kuwa mechi kama hizi zinaongeza vitu vingi vya muhimu kubwa likiwa kupanda kwenye viwango vya FIFA.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.


Post a Comment