SINGIDA UNITED YAKANUSHA FIFA KUMFUNGIA LYANGA, YATOA SABABU ZA MCHEZAJI HUYO KUTOKUONEKANA UWANJANI
Uongozi wa Klabu ya Singida United umekanusha juu ya kufungiwa na
FIFA kutojihusisha na Soka amshambuliaji wao Danny Lyanga kutokana na
usajili wake kuwa na utata huku wakitoa ufafanuzi juu ya suala la
mchezaji huyo.
Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema, Lyanga hajafungiwa bali mara baada ya kumsajili kutoka Fanja FC ya nchini Oman na kukamilisha kila kitu juu yake ikiwemo malipo kutokana na mchezaji huyo kuwa na mkataba wa mwaka mmoja zaidi na Klabu yake waliendelea kufuatilia hati yake ya uhamisho wa kimataifa (ITC) ambayo imekwama lakini mchezaji huyo yupo na timu akiendelea na mazoezi mpaka mwezi Julai itakapokamilika.
“Ukitamka neno kufungiwa ni neno kubwa na linaweza kuhatarisha kazi ya mchezaji mwenyewe, Danny Lyanga tulimsajili kwa kufuata taratibu zote kati ya Singida United na Fanja, alikuwa na mkataba na Fanja wa kumalizia mwaka mmoja kwahiyo tukaongea na Fanja wakaturuhusu kumtumia mchezaji kwa malipo na tukamlipa na tukapewa barua na kuendelea na usajili wa mchezaji, ” amesema.
Sanga amesema, Lyanga walimsajili dakika za mwisho za dirisha kufungwa kwasababu alikuwa anatokea CECAFA na timu ya Taifa hivyo alipowasili nchini wakakamilisha usajili wake na kilichokuja kukwama na ITC yake na wamepambana sana FIFA lakini wameambiwa Julai mwaka huu dirisha kubwa likishafunguliwa ndipo ITC yake itakuwa imefika.
Sanga amesema, Lyanga yupo kambini akiendelea na mazoezi na timu na watamtumia katika mashindano ambayo yapo mbele yao.

![]() |

Post a Comment