RUVU SHOOTING YAJA NA MFUMO MPYA WA "PAPASA", YASEMA ITABEBA POINTI TATU KWA MTIBWA SIKU YA JUMATATU BILA KUDHURIKA

Uongozi wa Klabu ya Ruvu Shoting umeitaka Klabu ya Mtibwa Sugar kuwa makini katika Uwanja wao wa nyumbani kwani dhamira yao kwa sasa ni kubeba pointi tatu na wamejipanga kupambana na kila hali ya ushindani watakayokutana nayo.




Afisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema, Mtibwa Sugar huwa hawawapi shida pindi wanapokukata na wamedhamiria kubeba pointi tatu kwa kila mchezo bila kujali wapinzani wao wapo katika kiwango gani katika Ligi hususani katika mchezo huo utakaopigwa Jumatatu ya Februari 19 Uwanja wa Manungu Mkoani Morogoro.


“Kikosi kipo vizuri sana, Morali ya vijana wetu ianzidi kupanda siku hadi sikuna sasa tunakwenda kukabiliana na Mtibwa Sugar kule Manungu Morogoro, ni mchezo ambao sisi kwanza huwa hautupi shida kwasababu Mtibwa wamekuwa kama wateja wetu wa siku zote, kwahiyo huwa hawatusumbui, nimemsikia rafiki yangu, ndugu yangu Thobias Kifaru akitamba kuwa anataka kututia adabu sasa sisi hatumtii adabu bali tunakwenda kumuadabisha, ” amesema.


Masau amesema, kasi na moto waliyonayo vijana wa Ruvu Shooting ni yahali ya juu sana kwani uwezo na ubora walionao wachezaji katika kucheza mpira niwaviwango vya juu sana hivyo wanahakika watawaaminisha Watanzania na mashabiki wao kuwa katika mechi zilizopita ambazo wamepata ushindi hawajabaatisha.


Masau amesema, wamedhamiria kumpiga Mtibwa Sugar akiwa nyumbani kwake ili kuondoka na pointi tatu na hata katika michezo inayofuata wanaamini watapambana bila kujali hali ya ushindani wa mpinzani aliyonayo.


Masau ameongeza kuwa wamekuja na mfumo mpya unaofahamika kama “PAPASA” ambao wanaimani watachukua ushindi bila kudhurika ili wazidi kupanda katika msimamo wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.


                                                            Kikosi cha Ruvu Shooting

No comments