TOTTENHAM VS ARSENAL WANATURUDISHA NYUMA HADI 1993
Mchezo unaosubiriwa na wengi hii leo ni kati ya Tottenham Hotspur vs
Arsenal mchezo ambao kwa mara ya kwanza mchezo huu unapigwa uwanja wa
Wembley tangu nusu fainali ya FA mwaka 1993.
Mara ya mwisho katika uwanja huu wa Wembley timu hizi mbili kukutana
Arsenal walishinda bao 1 kwa 0 mbele ya Tottenham huku bao pekee la
Arsenal likiwekwa kimiani na Tony Adams.
Arsenal wanaonekana watemi wa Tottenham kwani timu hizi mbili kwa
ujumla zimeshakutana mara 194 katika mashindano yote huku Arsenal
wakishinda mara 81 na Tottenham wakishinda mara 62.
Tottenham wanakwenda katika mchezo huu wakiwa hawajapoteza mchezo
hata mmoja katika mechi zao 8 zilizopita lakini michezo yao 5 ya mwisho
wamepata suluhu 3 katika ligi kuu ya EPL.
Rekodi sio nzuri sana kwa Arsenal kwani michezo 15 iliyopita ya EPL
vs timu 5 za juu Arsenal hawajashinda hata mmoja katika michuano ya EPL
na mara ya mwisho ilikuwa January 2015 vs Man City.
Mchezaji mpya wa Arsenal Pierre Aubameyang atakuwepo hii leo na
Aubameyang ana rekodi nzuri sana mbele ya Tottenham kwani katika michezo
minne ambayo amekutana na Arsenal amefanikiwa kuwafunga mara 4, moja
katika Champions League na matatu katika Europa.

Post a Comment