YANGA SPORTS CLUB KUWAKOSA WACHEZAJI HAWA KESHO KWENYE VPL DHIDI YA MAJIMAJI.
Timu ya Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga SC inatarajiwa kushuka
dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam kesho kuvaana na Majimaji FC huku
ikiwakosa nyota wake watatu ambao bado ni majeruhi mpaka sasa.
Hayo
yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na uongozi wa timu hiyo kupitia
moja ya kurasa zao za mitandao ya kijamii ambapo wamedai maandalizi
dhidi ya mchezo huo wa muendelezo wa VPL dhidi ya Majimaji FC
yamekamilika mpaka sasa.
"Tuko tayari kwa mchezo wa kesho, lakini hatutakuwa na
wachezaji watatu ambao ni Yohana Mkomola, Amisi Tambwe pamoja na Donald
Ngoma kutokana bado ni majeruhi hivyo hawatakuwa sehemu ya mchezo", imesema taarifa hiyo.
Kwa upande mwingine, timu ya Yanga imethibitisha kuwa ipo tayari kwa
ajili ya safari yake kuelekea Shelisheli kwenye mechi ya marudiano dhidi
ya St. Louis ambapo timu hiyo inatarajiwa kuondoka nchini Jumapili.

Post a Comment