WANACHOTAKIWA KUFANYA YANGA KWENYE MCHEZO WA MAREJEANO DHIDI YA SAINT LOUIS.

STRAIKA wa zamani wa Klabu ya Pamba na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Khalid Bitebo 'Zembwela' amewashauri Yanga kuwa iwapo watahitaji ushindi kwenye mechi yao ya marudio ya Klabu bingwa barani Afrika dhidi ya St. Louis wasipaki basi. 


Katika mchezo wa awali uliopigwa juzi jijini Dar es Salaam Yanga ikiwa nyumbani iliichapa St.Louis bao 1-0, ambapo inatarajia kucheza mechi yake ya marudio ugenini Februari 21 mwaka huu.

Bitebo alisema kuwa katika mechi ya marudio,Yanga wanapaswa kwenda na mpango mkakati wa kushambulia zaidi na kulinda kwa tahadhari kwani bao moja walilopata nyumbani bado haliwatoshi.

Alisema kuwa hata kiwango walichoonyesha kwenye mchezo huo wa Jumamosi,hakikuwa cha kuridhisha,hata safu ya ushambuliaji ilionekana kutotulia kufanya kile walichotegemea wadau wa soka.

“Lazima benchi la ufundi na timu kwa ujumla waende na makakati wa kusaka ushindi,bao moja walilopata bado wana kazi ngumu,wapinzani wao walikuja na tahadhari kubwa”alisema Bitebo.

Nyota huyo wa zamani aliongeza kuwa kwa jinsi Yanga walivyocheza,ilionekana wazi matokeo kuwa suluhu na kwamba bao walilopata ilikuwa bahati tu. 

Alisema kuwa anaamini Yanga wanao uwezo wa kufuzu iwapo watarekebisha kasoro ambazo zilitokea kwenye mchezo uliopita,hivyo wakaze kweli kweli. 

“Umakini kwa washambuliaaji ulikuwa mdogo sana,kwahiyo benchi la ufundi liangalie mapungufu yote ili mechi ya marudio ugenini waweze kupata matokeo mazuri na kusonga mbele”alisema Straika

No comments