MAYANGA ASEMA HAWAHOFII ALGERIA HATA KAMA WALISHAWAHI KUFUNGWA 7-0, NA HICHI NDICHO WANACHOKIHITAJI LEO
Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania
“Taifa Stars” kimesema licha ya kuwa na historia mbaya ya
kufungwa na Algeria bao 7-0 lakini leo kimejipanga kwaajili ya
ushindi dhidi ya wapinzani wao hao ikiwa ni mchezo wa kirafiki wa
kimataifa wa kalenda ya FIFA utakaopigwa mjini Algiers, Algeria ili
kupanda katika viwango vya FIFA.
Kocha Mkuu wa Timu hiyo Salum mayanga
amesema, kikosi kipo imara kwaajili ya mchezo huo utakaopigwa majira
ya saa mbili usiku kwa saa za hapa nyumbani na wanaamini kutokana na
maandalizi waliyonayo japo niyamuda mfupi lakini yataweza kuwapa
matokeo mazuri ndani ya Dakika 90.
“Timu ya Taifa stars ipo kwenye hali
nzuri tangu jana tulipomaliza mazoezi jana na leo tunajiandaa kabla
ya mechi yetu ambayo itachezwa majira ya saa 12 jioni kwa saa za huku
Algreria na kwatanzania ikiwa ni saa mbili usiku, ” amesema.
“Nimatumaini yetu tutacheza mchezo
mzuri na kuweza kupata ushindi katika mchezo wa leo jambo ambalo
litakuwa zuri kwetu, kwakifupi kila mchezaji anamorali na
tutakapomaliza mchezo huo, kesho timu itaanza safari yakurejea
nyumbani, ” amesema.
![]() |
| Kikosi cha Timua ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" |

Post a Comment