VALVARDE AMEKIRI KUWA NA WAKATI MGUMU MBELE YA CHELSEA DARAJANI USIKU WA LEO.
Kocha mkuu wa Barcelona, Ernesto Valverde amesema kuwa alitamani timu ya
Chelsea ingeshinda katika kundi lake na kuongoza ili tu asikutane nayo
katika hatua hii ya 16 bora kwakuwa kila wanapokutana wanakuwa na wakati
mgumu kwao dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Uingereza.
Akizungumza na vyombo vya habari, Valverde amesema alitarajia kuikwepa
Chelsea katika hatua hizi za awali lakini amesisitiza kuwa wachezaji
wake wapo tayari kwajili ya mchezo huo.
“Tulitarajia Chelsea wangeshinda na kuongoza kundi na wangefanikiwa
hilo tusingekutana nao, lakini tunakuwa na wakati mgumu sana
tunapokutana nao,” amesema Valverde.
‘”Wamekuwa katika kiwango kizuri Hazard, Morata, Pedro na Willian
wana ubora wa hali ya juu hapa nawazungumzia mabingwa wa sasa wa ligi ya
Uingereza ambao tunakwenda kukutana nao.”
Timu hizi zilitoka sare michezo yake ya mwisho na kumaliza nafasi ya
pili wakati Chelsea wakiwa nyuma ya Roma katika kundi C na sasa
wachezaji wa Barcelona wapo katika dimba la Stamford Bridge wakijiandaa
dhidi ya wenyeji wao mchezo unaotarajiwa kupigwa leo siku ya Jumamosi
usiku.
Post a Comment