YANGA YAANIKA JESHI LA WATU 20 KWA AJILI YA SPORTPESA SUPER CUP


Klabu ya Yanga imetangaza wachezaji 20 watakaoshiriki michuano ya SportPesa Super Cup na wanatarajia kuondoka leo kuelekea Kenya kwa ajili ya mikiki mikiki hiyo itakayoanza wiki ijayo.

Kikosi kamili cha Yanga kitakacho ondoka leo ni makipa Youthe Rostand na Ramadhani Kabwili.

Walinzi ni Hassan Kessy, Hajji Mwinyi, Abdullah Shaibu, Said Juma na Pato Ngonyani.

Viungo ni Baruan Akilimali, Pius Buswita, Maka Edward, Thaban Kamusoko, Said Mussa, Juma Mahadhi, Papy Tshishimbi na Raphael Daud.

Washambuliaji Ibrahim Ajib, Yohana Mkomola, Matheo Anthony Amis Tambwe na Yussuf Mhilu.

Katika kikosi hicho Yanga imewaacha nyota wake Kelvin Yondani, Obrey Chirwa na Andrew Vicente 'Dante's.

Wachezaji wengine ambao hawaja jumuishwa katika kikosi hicho ni Juma Abdul, Gadiel Michael, Nadir Haroub, Geofrey Mwashiuya na Emmanuel Martin.

No comments