MUDA WA WAJUMBE WA MKUTANO WA FIFA TANZANIA KUANZA KUWASILI SIKU HII.



Wajumbe wanaotarajia kushiriki mkutano wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA wanatarajia Kuanza kuwasili kesho kwaajili ya mkutano huo utakaofanyika Februari 22 Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.


Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini TFF Mario Clifford Ndimbo amesema,  maandalizi kwaajili ya mkutano huo yameshakamilika na wanaendelea na mawasiliano ili kujua Rais wa FIFA ambaye atawasili na ndege na ndiye mjumbe wa mkutano huo atawasili lini na muda gani. 

"Rais anawasili kwa ndege binafsi kwahiyo tunafanya mawasiliano kujua siku na muda rasmi atakaowasili,  na maandalizi yameshakamilika hivyo tunatarajia kila kitu kitakwenda kama kilivyooangwa,  " amesema. 

Wakati huohuo TFF kupitia kwa afisa Habari wake Mario Clifford Ndimbo amesema,  mara baada ya ungwe ya Kwanza ya uuzwaji wa tiketi za kushuhudia Kombe la Dunia, FIFA imeongeza tiketi kwa mashabiki watakaohitaji kushuhudia Fainali hizo zitakazofanyika Mwezi Juni mwaka huu nchini Russia.

“Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limetuongeza tiketi Tanzania za kushihudia mechi za Kombe la Dunia mwaka huu pale Russia, ikumbukwe kuwa mwanzoni Tanzania tuliletewa tiketi 290 kabla ya zoezi kuweka kufungwa Mwezi Januari, lakini sasa wametufungulia ungwe nyingine ya tiketi hizo kwa maana kwamba kwa Matanzania yoyote anayetaka kushuhudia Fainali hizo za Kombe la Dunia basi awasiliane na Idara ya mashindano ya TFF na ungwe hii inataraji kumaliziak Machi 12 mwaka huu kwamaana zoezi litafungwa, ” amesema.

No comments