ANACHO KIJUTIA GIROUD TANGU ALIPO ONDOKA ARSENAL NI HIKI.
Mshambuliaji Olivier Giroud amesema ameondoka Arsenal akiwa anajutia kitu kimoja tu, kushindwa kubeba taji la Ligi Kuu England akiwa na miamba hiyo ya Emirates.
Mshambuliaji huyo Mfaransa kwa sasa yupo Chelsea alishinda mataji matatu tu ya Kombe la FA
alipokuwa na kikosi cha Arsenal kabla ya kutimkia Stamford Bridge kwenye dirisha lililopita la usajili kwa ada ya
Pauni 18 milioni ili kupata nafasi ya kucheza
akaitumikie Ufaransa kwenye Kombe la Dunia.
Kwenye mahojiano aliyofanyiwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea na
Arsenal, ambaye pia ni Mfaransa
mwenzake, William Gallas, kwamba anajutia nini baada ya kuondoka Emirates,
Giroud alisema: “Kujutia? Ni jambo
lilelile lililozoealeka, si gumu kulifikiria.
“Sijui kama hiyo ni kujutia au vipi, lakini nasikitika kumaliza
maisha yangu kwenye kikosi cha Arsenal bila
ya kutwa taji la Ligi Kuu England kitu ambacho ndiyo lengo la kwenda kujiunga
na timu hiyo.
“Sawa unaweza kusema juu ya muda kwamba ni mchache, lakini hiyo
ndiyo ilikuwa dhamira yangu. Hata hivyo
ndoto hazijafutika, bado nipo kwenye Ligi Kuu England na sasa nipo Chelsea.”
Post a Comment