MAJIMAJI: LAZIMA TUIFUNGE SIMBA LEO



Licha ya kuwa kwenye hali mbaya katika msimamo wa ligi timu ya Majimaji imejiapiza kutoka na ushindi katika mechi ya leo ya kufungia msimu dhidi ya Simba.

Majimaji ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo ikiwa na pointi 24 ikiwa katika janga la kushuka daraja na hata kama wataifunga Simba leo bado watasubiri matokeo kati ya Ndanda FC dhidi ya Stand United.

Meneja wa timu hiyo, Godfrey Mvula amesema kwa namna yoyote itakavyokuwa wamejipanga kuifunga Simba hata kama watashuka daraja.

Simba imepeleka kikosi cha wachezaji wengi ambao walikuwa hawapewi nafasi msimu kitu ambacho kinaweza kuwafanya Majimaji kupata ushindi katika mchezo huo wa nyumbani.

"Iwe jua au mvua Simba itafungwa leo hakuna namna nyingine halafu tunaiombea mabaya Ndanda ifungwe ili tubaki kwenye ligi msimu ujao," alisema Mvula.

Kocha wa timu hiyo, Habib Kondo alinukuliwa akisema hawana nafasi ya kubaki kwenye ligi msimu ujao akifananisha na ngamia kupenya kwenye tundu la Sindano.

No comments