MENDIETA AMTAHADHARISHA GRIEZMANN
Gaizka Mendieta amemuonya mshambuliaji Antoine Griezmann kuwa atacheza nyuma ya kivuli cha Lionel Messi kama atakubali kujiunga na Barcelona.
Nyota huyo wa Atletico Madrid ana husishwa kutaka kujiunga na miamba hiyo ya La Liga ambapo alikaririwa akisema mustakabali wake utajulikana kabla ya kuanza michuano ya kombe la dunia.
Mendieta anaamini kama atajiunga na Barca atafunikwa na kivuli cha Messi hivyo atashindwa kung'ara tena.
"Nadhani itakuwa muhimu kwake kubaki Atletico kuliko kwenda Barcelona, akienda kule kuna mechi atawekwa benchi kwakua kuna wachezaji bora wengi.
"Kubaki Atletico itakuwa vizuri kwake kwakua wachezaji wenzake wanamtazama yeye muda wote lakini akienda Barcelona wachezaji wanamtazama Messi kwanza," alisema Mendieta.
Griezmann 27, ameiwezesha Atletico kutwaa taji la Europa msimu huu na sasa yupo kwenye kikosi cha Ufaransa kinacho jiwinda na fainali za kombe la dunia nchini Urusi.
Post a Comment