HIKI NDICHO ANACHOKIAMINI MSUVA MARA BAADA YA BENCHI LA UFUNDI LA TAIFA STARS KUFANYA ONGEZEKO LA WACHEZAJI WANAOCHEZA LIGI YA ZANZIBAR
Winga wa
Kimataifa Mtanzania anayeitumikia Klabu ya Difaa El Jadida ya nchini
Morocco Simon Msuva amesema uamuzi wa benchi la ufundi la Timu ya
Taifa ya Tanzania kufanya ongezeko kwa kuchukua wachezaji wanaocheza
Ligi ya Zanzibar ni mzuri na wanaamini watashirikiana ili kuweza
kuipa timu ya taifa matokeo mazuri katika michezo ya Kirafiki ya
Kalenda ya FIFA dhidi ya Algeria na DR Congo na hata katika
mashindano mbalimbali.
Msuva amesema
kuwa, anaimani na wachezaji wa Zanzibar kwani kwa kushirikiana
wataweza kuitangaza zaidi Tanzania katika ramani ya Soka.
Msuva amesema,
anaamini benchi la ufundi lilikaa na kuangalia uwezo wa wachezaji
waliowachagua kwani kila mchezaji anauwezo na wanaamini hata katika
timu watakazokutana na zo wataweza kufanya vizuri zaidi.
Msuva amesema,
Timu ay Taifa ni yawachezaji wote na hata kama mchezaji ajaitwa
katika kikosi hana haja ya kukata tamaa kwani kila mchezaji anamuda
wake wa kuchezea timu ya Taifa kikubwa ni kufanya jitihada katika
vilabu ili waweze kuonekana.
Msuva ameongeza
kwa kuwataka wachezaji wa hapa nchini kuongeza jitihada katika soka
na kutokukata tamaa ili kuweza kutoka nje ya mipaka ya Tanzania
kwaajili ya kukuza soka lao kwamanufaa ya timu ya Taifa.
Msuva amesema,
hiki ndicho kipindi cha wachezaji wengi zaidi kutoka kwaajili ya
kucheza soka la kulipwa kwani wanapofanikiwa kutoka wachezaji wengi
inasaidia kwa kiasi kikubwa timu ya Taifa kuweza kufanya vizuri kwani
inakuwa na wachezaji wazuri na wenye viwango.

Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.
Post a Comment