CHUJIO KUPITA TENA NGORONGORO HEROES MARA BAADA YA KUMALIZANA NA MOROCO KESHO PAMOJA NA MSUMBIJI MACHI 21



Kikosi cha Timu ya Taifa ya vijana walio na umri chini ya Miaka 20 “Ngorongoro Heroes” kesho kinashuka dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuvaana na Timu ya Taifa ya Taifa ya Moroco katika mchezo wa kwanza wa Kirafiki ikiwa ni maandalizi kwaajili ya kuwania kufuzu AFCON U20.

Kocha Ninje amesema, mchezo huo pamoja na ule dhidi ya Msumbiji utakaopigwa Machi 21 utatumika kama mchujo wa kupata kikosi cha wachezaji angalau 23 watakaoweza kuanza maandalizi ya mbio za kuelekea katika michuano ya AFCON ambapo mchezo wa kwanza wataanza dhidi ya DR Congo Machi 31 katika uwanja wa Taifa kabla ya ule wa marudiano utakaofanyiika baada ya wiki mbili jijini Kinshansha.

Kikosi kipo imara na leo tunafanya mazoezi ya mwisho kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa kesho, Tumepata michezo miwili ya Kimataifa na ni vizuri kwenda kwenye mashindano makubwa ikiwa umeshaona kikosi chako kinavyocheza kwahiyo nashukuru sana na nategemea kuwajua vizuri wachezaji wangu na nitajua nitumie vijana wangapi katika mchezo wa Congo, ” amesema.



                                        Kikosi cha Ngorongoro Heroes

Kocha Ninje amesema, mpaka sasa anakikosi cha wachezaji 30 kwahiyo hawezi kwenda na wachezaji wote bali anachagua vijana angalau 23 ambao anaamini wataweza kuanza kampeni za kuwania kushiriki AFCON.

Nitajaribu kuangalia katika kikosi cha kesho na kwenye mchezo dhidi ya Msumbiji pia nitaangalia halafu tutakaa na kuangalia wachezaji wapi tuwapunguze lakini sio kwa mabaya kwani tutawapunguza waende kwenye klabu zao lakini muda wowote pia tutaweza kuwatumia, ” amesema.

Kila mchezaji yupo vizuri kwahiyo najua tutapata wakati mgumu katika kuchagua wachezaji hao ninaowahitaji ila vipo vigezo pia, ” amesema.

Kocha Ninje amesema, kikosi amekikuta kikiwa katika hari nzuri ya kupambana hivyo imempa urahisi pia wa maandalizi kwaajili ya michezo iliyopo mbele yao.
            

                                  Kocha wa Ngorongoro Heroes, Amy Ninje

Follow us on Instagram @Tiktaktz ili uwe wa kwanza kupata taarifa mpya za michezo yote ndani ya nchi na nje ya nchi.

No comments