TAIFA STARS KUCHEZA NA MATAIFA HAYA KWENYE KALENDA YA FIFA MWEZI HUU.

Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza kuwa timu ya taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars itacheza mechi mbili za Kalenda ya FIFA ambazo ni dhidi ya Algeria na DR Congo. 



Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari TFF imebainisha kuwa mechi hizo za kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa FIFA kwa mwezi Machi zitachezwa ndani ya wiki moja.

Taifa Stars itacheza na Algeria Machi 22, 2018 nchini Algeria kisha kucheza na DR Congo Machi 27, 2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Tanzania.

Pamoja na kutaja tarehe ya michezo hiyo lakini TFF haijatangaza ni lini kikosi cha Taifa Stars kitatajwa na timu kuingia kambini kwaajili ya maandalizi ya mechi hizo ambazo ni muhimu.

Tanzania imekuwa haifanyi vizuri kwenye viwango vya FIFA ikiwa inazidiwa na nchi zingine za Afrika mashariki kama Uganda. Kenye na Rwanda.


No comments