CHAMA CHA RIADHA TANZANIA (RT) KIMETAKIWA KUSITISHA TOZO HII NA BARAZA LA MICHEZO TANZANIA.
Baraza la michezo nchini (BMT)
limekiagiza Chama cha riadha Tanzania (RT) kusitisha tozo la ada mpya za mbio
ndefu (Marathon) na itumike ada ya zamani ili kuepisha kutokuelewana baina ya
waendeshaji wa mbio hizo na RT.
Katibu mkuu wa BMT Mohamed Kiganja
amesema, mara baada ya RT kukutana na wadau wa Marathon Oktoba mwaka jana
na kuwaelekeza mabadiliko ya ada kulitokea sintofahamu baina yao na kupelekea
waendeshaji wa Marathon kuandika barua serikalini wakilalamikia ongezeko la ada
ambalo lilipanda mara mbili hivyo wao wakiwa ni Serikali imewalazimu kutoa
uamuzi huo huku wakipanga kukutana na wadau pamoja na chama ili kutengeneza
namna bora ya kuratibu mbio hizo.
"Waendeshaji wa Marathon
walikiwa wakilipa baadhi ya mbio kiasi cha shilingi milioni mbili na zikapanda
mpaka milioni sita, kwahiyo kama Serikali hatuwezi kulifumbia macho na
tunaamini maamuzi haya tunaamini hakutokuwa na migogoro isiyo na sababu, "
amesema.
Kiganja amewataka waandaaji wa mbio
hizi kuwa mara baada ya kusitoshwa ada mpya wanatakiwa kufuata sheria kwani
wengi wao bafo hawajasajiliwa.
Kiganja ameongeza kuwa Machi 05
mwaka huu mara baada ya kumalizika kwa mbio za Kili "Kili Marathon"
watakutana pande zote wakiwemo BMT, RT na waandaaji ili kujadili suala
hilo.
Kiganja ameongeza kwa kuwataka
waandaaji wote kutumia kamati za michezo za mikoa kama sheria zinavyotaka
Post a Comment