AZAM YAIFUNZA YANGA JINSI YA KUSAKATA KABUMBU


Timu ya Azam imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga katika mchezo ambao walitandaza soka safi mbele ya mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu.

Azam walionekana kuhitaji ushindi katika mchezo huo kutokana kushambulia kwa kasi wakicheza kwa malengo ambayo yaliwafanikisha kupata pointi tatu.

Matokeo hayo yameifanya Azam kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi baada ya kufikisha pointi 58 alama 11 nyuma ya mabingwa Simba.

Yanga ilionekana kushindwa kuhimili vishindo vya Azam ambao walikuwa na dhamira ya kutafuta alama tatu.

Katika mchezo huo mabao ya Azam yalifungwa na Yahya Zayd, Shaban Idd na Salum Abubakar 'Sure Boy' wakati lile la Yanga akijifunga mlinzi Abdallah Kheri.

Yanga imemaliza ligi vibaya kufuatia kupoteza mechi tano katika mechi sita zilizopita.

No comments